Ugumu wa Wanaume wengi kuomba MSAMAHA.

By George Allen Msumai
2nd May, 2020

Kwa Nini Wanaume wengi ni Wagumu Kuomba Msamaha?

Ni ukweli usiopingika wanaume wengi hudhani wao kuomba msamaha kwa wanawake ni kujishushia hadhi au kuonesha udhaifu. Wengi hujitutumua na kuishia kusema ‘POTEZEA TU, au VUNGA, au YAISHE au KAUSHA’. Sasa sijui nini kinakaushwa hapa, ni mishikaki au chipsi? Sijuwi mimi.


Kwa haraka mtu anaweza kudhani hii ni kwenye ndoa tu, lakini hata kwa vijana ambao hawajaoa, inaweza kutokea mkakwaruzana au kukwazana na msichana yoyote mnayesoma naye au rafiki wa kawaida ambapo wanaume wengi hupata ukakasi kutamka neno ‘nisamehe dada yangu, nisamehe rafiki yangu’. Huu ni ujinga, na ujasiri wa hasara kwa maana haijaandikwa kuwa wanawake tu ndio watakuwa wanakosea. Ni vyema wanaume kujifunza kuomba msamaha pale unapomkosea mwanamke yoyote ili isikupe shida hata ukiingia kwenye ndoa na kufanya kosa fulani kwa mkeo, kisha kuanza kuona ukakasi kuomba msamaha. Ukiulizwa kitu ambacho unajua kabisa umefanya kosa, unaanza kujitutumua kuonesha hasira na kutengeneza mazingira kuwa kwa wanaume ni kawaida kufanya hicho kitu, hapana, hiyo sio kweli.


Kwa mwanaume kuomba msamaha kwa mwanamke hakupunguzi uanaume wako wala kukudisqualify kutoka kwenye nafasi uliyopo, bali ni tendo la kijasiri na ukomavu kifikra , kimtazamo na maamuzi. Ile amani anayopata mwanamke baada ya kuombwa msamaha ni baraka kwako. Halafu masikini ya Mungu wanawake hata hawaoni kazi kusamehe, hasa ukionesha kweli umeelewa kosa. Mara nyingi kwasababu ya kujiona dhaifu hujikuta wanasamehe hata bila kuombwa msamaha, sawa hili ni zuri sana kuwa nalo hata kwa wanaume.

This site was designed with Websites.co.in - Website Builder

WhatsApp Google Map

Safety and Abuse Reporting

Thanks for being awesome!

We appreciate you contacting us. Our support will get back in touch with you soon!

Have a great day!

Are you sure you want to report abuse against this website?

Please note that your query will be processed only if we find it relevant. Rest all requests will be ignored. If you need help with the website, please login to your dashboard and connect to support